Ijumaa, 2 Oktoba 2015

BOND AFUNGUKA MAZITO KUHUSU WASTARA JUMA

 Mcheza filamu za kitanzania na mtangazaji wa kipindi cha action and cut ,Bond bin sinan amesema amesema 27.09.2014 ndio tarehe ambayo mama yake mzazi amefariki dunia,lakini cha kushangaza tarehe hiyo hiyo miaka tofauti mwenyezi mungu amemleta mcheza filamu mwenye jina kubwa nchini Wastara Juma Issa ambae ndio mpenzi wake kwasasa

akifunguka kiafrika bila hofu yoyote Bond ameshindwa kuzuia furaha yake na kuandika mazito kupitia ukurasa wake wa facebook



Siku ya Tarehe 27 mwezi wa 9 mwaka 1994 ni siku Mama yangu alinifariki na kuniacha mpweke na nikajiona kuwa sitakuwa na furaha. 

Lakini tarehe hiyo hiyo 27/09 kasoro mwaka alizaliwa binti mmoja mzuri wa ajabu mwenye sifa nyingi nzuri ambazo kila mtanzania anazijua kuanzia kazi, upendo, huruma, uvumilivu na ujasiri kwakweli mungu hajawahi kukosea wala hatokosea kufanya maamuzi

Kwani humpa amtakae na humnyima amtakae na yote ikiwa ni kwa kheri zake
Asante mungu kwa kunijaalia kunipa na kumjua huyu mwanamke mzuri

Wastara ateseka atamani kuua!

Hii ni habari ya kusikitisha! Staa wa sinema za Kibongo, Wastara Juma anadaiwa kuteswa na kitu kilichoitwa pepo mbaya ambaye humsababishia hasira kali hasa anapokosewa ambapo anapokumbwa na hali hiyo, hujikuta anataka kuua.

TUJIUNGE NA CHANZO
Sosi aliye karibu na staa huyo aliyezungumza na Ijumaa mapema wiki hii alinyetisha habari hiyo ambayo mbali na kumtesa Wastara, pia inaitesa familia yake kwani mara nyingi huamua kukaa mbali naye pindi anapokutwa na hali hiyo.Sosi huyo alinyetisha kwamba, kuna kipindi hali hiyo ikimkuta Wastara huwa na stress (msongo) wa mawazo.
HARUFU YA DAMU, KUTAKA KUUA MTU
Ilidaiwa kwamba, akiwa katika hali hiyo, Wastara huunguruma kama mtu aliyepandwa na kitu na husikika akisema kuwa anasikia harufu ya damu na kwamba anataka kuua mtu.“Yaani unaambiwa hali hiyo ikishamtokea huwa tunajifungia ndani na kumpisha anahangaika mwenyewe kwani tunahofia jambo baya la mauti,” alisema sosi huyo ambaye ni mtu wa ndani ya familia.
KUPOROMOSHA MATUSI
Chanzo hicho kiliendelea kudai kwamba, mbali na kutaka kuua, pia Wastara huporomosha matusi mfululizo ambayo akiwa kawaida hawezi kuyatoa, kitendo kinachoshangaza, kwani anaweza kutukana kuanzia asubuhi hadi jioni.


Baada ya kuzinyaka habari hizo, mwanahabari wetu alimwendea hewani Wastara ili kujua kinachomsumbua ambapo alifunguka kwa masikitiko:
“Sijui ni nani amewafikishia habari hizi kwani zinanisikitisha sana lakini naomba watu watambue kuwa nina tatizo ambalo sijajua nitalimaliza vipi.“Wala huyo mtu hajakwambia uongo, ni kweli kwa sababu nina damu mchanganyiko na nikikasirika nyumba nzima wanajifungia ndani.“Ninajitahidi sana kujibadilisha ili niwe kawaida lakini inashindikana. Ndiyo maana huwa napenda kukaa kimya sana kwani najijua nina tatizo.
MCHANGANYIKO WA DAMU
“Nina mchanganyiko wa damu ya Kimasai, Kiarabu, Kinyamwezi, Kihindi, Kinyarwanda na Kigunya ndiyo maana nahisi nina tatizo kubwa ambalo naomba Mungu anitatulie.
“Kuna wakati huwa natamani kumpasua mtu pale anaponiudhi na asiamke kabisa ndiyo roho yangu inaridhika.

ALA MARA TANO, SODA ISHIRINI KWA SIKU
“Ninapokuwa na tatizo hilo ambalo mara nyingi huambatana na ‘stress’ zilizonizidi, huwa najikuta nakula sana kama mara tano kwa siku na huwa nakunywa soda kama ishirini hivi.“Mtu akiniona nanenepa ni kwa sababu ya stress za maisha ndiyo husababisha hali niliyonayo.
AJITAHIDI KUSALI
“Huwa najitahidi kusali sana ili nione kama hali hii itaniondokea, naamini ipo siku nitakuwa sawa na matatizo yote yataisha. Pia ni jambo la kuombewa sana dua.
TUJIKUMBUSHE
Wastara amekuwa akikumbwa na mikasa ya kila aina kama ajali za mara kwa mara hivyo kujiona mwenye mikosi ambapo mashabiki wake wamekuwa wakimshauri kusali sana ili aepukane na mikosi hiyo.